Connect with us

Soka

Kocha Simba Aipa Tano Gsm

Kocha wa zamani wa klabu ya Simba sc Jamhuri Kihwelu “Julio” ameipongeza kampuni ya Gsm baada ya kukubali kuendelea kuisaidia klabu ya Yanga baada ya kuandika barua ya kusitisha mambo yote yaliyopo nje ya mkataba.

Julio amesema licha ya kampuni hiyo ina malengo yake ya kibiashara, ila inachokifanya kuisaidia timu hiyo nje na mkataba ni zaidi ya mapenzi ambayo yanapaswa kuungwa mkono ili kuifanya timu iendelee kuwa na ufanisi na kuipa thamani yake timu hiyo.

“GSM ni mfanyabiashara anafanya vitu kwa faida, lakini kwa mapenzi yake aliamua kuwasaidia zaidi ya mkataba wake na alichowekeza na unajua Yanga ilikuwa na changamoto nyingi kuanzia usajili, mishahara na mengineyo ya ziada wanapaswa kuungwa mkono na sio kuwabughudhi,” Alisema Kocha huyo aliyewahi kuifundisha klabu ya Simba sc mara kadhaa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka