Connect with us

Soka

Kitambi Kupigwa Msasa

Kocha msaidizi wa klabu ya Simba Dennis Kitambi amepata nafasi ya kushiriki mafunzo ya ukocha ya Uefa ambayo yatatolewa nchini na wataalamu kutoka Denmark kuanzia disemba 2-10 mwaka huu.

Kitambi ambaye kwa sasa ndiye msimamizi wa masuala yote ya kiufundi ndani ya klabu hiyo baada ya kocha mkuu kusimamishwa atahudhuria mafuzno hayo ili kuongeza uwezo zaidi wa kazi.

Mpaka sasa haijajulikana kocha ambaye atakaimu nafasi ya kitambi klabuni hapo huku meneja wa klabu hiyo Patrick Rweyemamu akithibitisha kocha huyo kuomba ruhusa ya kuhudhuria mafunzo hayo huku akisema suala la nani atarithi majukumu linashughulikiwa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka