Connect with us

Soka

Kipa Kmc Kikaangoni

Uongozi wa klabu ya KMC ya Dar kupitia kwa Mwenyekiti wa Klabu hiyo Kheri Nassoro umesema utamchukulia hatua za kinidhamu Golikipa wa Klabu hiyo Jonathan Nahimana Raia wa Burundi kutokana na kauli yake ya hivi karibuni ya kusema anatamani kucheza Simba.

Kipa huyo alisema maneno hayo wakati bado akiwa na mkataba na klabu ya KMC hali iliyomfanya Nassoro kushangazwa sana na kauli hiyo kutoka kwa golikipa wa kimataifa kutoka nchini Burundi.

Licha ya kipa huyo kutamka kutaka kujiunga na Simba sc pia imebainika baadhi ya timu barani Afrika zinamnyemelea ikiwemo Horoya na baadhi ya klabu nchini Burundi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka