Connect with us

Soka

Kilimanjaro Waua 9

TIMU ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake ‘Kilimanjaro Queens’ leo imeanza kwa kishindo michuano ya CECAFA uwanja wa Chamazi kwa ushindi wa mabao 9-0 dhidi ya Sudan Kusini.

Mchezo huu umevunja rekodi ya mabao yaliyofungwa na Burundi mbele ya Zanzibar ambao walikubali kulala kwa mabao 5-0 uwanja wa Chamazi.

Mwanahamis Omari aliandika mabao yake matatu na kusepa na mpira wake akifunga mabao dakika ya 18,43 na 42, Donesia Minja alifunga bao lake moja matata kwa guu la kushoto dakika ya 33 huku Opa akipachika mabao mawili dakika ya 50 na 85 Stumai naye alipachika mawili dakika ya 48 na 52 aliyefunga bao moja mwingine alikuwa ni Juditha dakika ya 55.

Mchezo wa leo umeweka rekodi ya aina yake kwa Kili ambao ni mabingwa watetezi kuotea mara 23 na Sudan waliotea mara mbili pekee huku Mwanahamis Omary akikosa nafasi tatu za wazi kipindi cha kwanza kwa kile alichoeleza kuwa ni presha ya mchezo.

NB.Habari hii ni kwa msaada wa Salehejembe

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka