Connect with us

Soka

Kilimanjaro Queens Yamfunga Burundi

Timu ya taifa ya Wanawake ya Tanzania Bara(Kilimanjaro queens) imeibuka na ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya Burundi katika mchezo wa michuano ya kombe la chalenji kwa wanawake inayoendelea nchini.

Hii ni mechi ya pili kwa Kilimanjaro queens kuibuka na ushindi baada ya hapo awali kuwafunga Sudan Kusini jumla ya mabao 9-0 mchezo uliofanyika uwanjani hapo chamazi.

Mabao ya Kilimajaro katika mchezo wa leo yalifungwa Donisia Minja dakika za 35′ na 75′ huku Asha Rashid pia akifunga dakika ya 72 na Mwanahamis Omary dakika ya 86 na kufanya timu hiyo kuwa na magoli 13 ya kufunga katika michezo miwili.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka