Connect with us

Soka

Kaze Atwaa Tuzo Oktoba

KOCHA wa Young Africans SC ya Dar es Salaam, Cedric Kaze, amechaguliwa kuwa Kocha Bora wa mwezi Oktoba msimu wa 2020/21.

Kaze aliwashinda Aristica Cioaba wa Azam FC na Francis Baraza wa Biashara United ambapo Kaze aliiongoza Yanga katika michezo mitatu na kushinda yote. Yanga chini ya Kaze ilizifunga Polisi Tanzania, KMC na Biashara United na kupanda kutoka nafasi ya tatu hadi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom.

Cioaba aliiongoza Azam kushinda michezo mitatu, sare moja na kupoteza moja, huku Baraza akiiongoza Biashara kushinda michezo mitatu na kupoteza miwili ikipanda kutoka nafasi ya saba hadi ya nne.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka