Connect with us

Soka

Kaseja Ala 10m za Makonda

Kufuatia kuonyesha kiwango bora katika mchezo wa kimataifa dhidi ya Burundi Kipa Juma Kaseja amezawadiwa fedha taslimu shilingi milioni 10 na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda.

Makonda ametoa ahadi hiyo jana kupitia ukurasa wake wa mtandao wa instagram baada ya mchezo kumalizika kwa taifa stars kufanikiwa kuingia hatua ya makundi ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia nchini Qatar mwaka 2022.

Kaseja licha ya kufanya vizuri katika dakika tisini za mchezo hasa akipangua mpira wa hatari uliopigwa kunako dakika ya 87 ya mchezo alifanya vyema zaidi wakati wa mikwaju ya penati baada ya kucheza penati ya kwanza ya Burundi huku pia akikaribia kuicheza penati ya pili iliyopigwa na Saido Berahino  iwapo ingekua imelenga lango.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka