Connect with us

Soka

Kaseja Aibukia Twiga Stars

Kipa wa timu ya taifa ya Tanzania(Taifa stars) Juma Kaseja ameibukia kwenye mazoezi ya timu ya taifa ya wanawake Tanzania (Twiga stars) akiwanoa makipa wa timu hiyo.

Kipa huyo mkongwe aliyetoka kuisaidia Taifa stars kushinda mchezo dhidi ya Sudan na kufanikiwa kukata tiketi ya fainali za michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani ameshiriki mazoezi ya timu hiyo inayojiandaa na michuano ya chalenji ambayo itafanyika nchini kuanzia novemba 14-23 desemba.

“Mimi ni Mtanzania, na nina jukumu la kuisaidia Tanzania, nimemaliza majukumu ya Stars, jana (juzi) nimecheza mechi (JKT Tanzania vs KMC), na leo nimeamua kuja kufanya mazoezi na dada zetu, mara nyingi nimekuwa nikiwasaidia, ili waweze kutimiza ndoto zao,” alisema Kaseja.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka