Connect with us

Soka

Kapombe Asaini Miwili Simba

Beki wa Simba sc Shomari Kapombe amesaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kusalia klabuni hapo baada ya mkataba wa awali wa miaka miwili kumalizika mwezi huu.

Beki huyo mwenye uwezo wa kucheza nafasi zote za idara ya ulinzi pamoja na kiungo amesaini mkataba mpya licha ya kutokuwa na misimu mizuri tangu ajiunge klabuni hapo ambapo amekua akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara tangu ajiunge akitokea Azam Fc ambapo nako hakuwa na msimu mzuri baada ya kuugua kwa muda na kutibiwa nchini Afrika ya kusini.

Hivi karibuni beki huyo alizua sintofahamu baada ya taarifa kudai amejitonesha majeraha akiwa katika kambi ya timu ya taifa inayojiandaa na michuano ya Afcon japo mwenyewe alikanusha na kusema hajajiunga na timu hiyo kwa kuwa hajapona vizuri na ana programu maalumu ya matibabu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka