Connect with us

Soka

Kapombe Ajiengua Stars

Beki wa timu ya Simba sc Shomari Kapombe amejitoa kuichezea timu ya taifa ya Tanzania (Taifa stars) kutokana na kuandamwa na majeraha ya mara kwa mara hali inayotishia uhai wa soka lake.

Kapombe aliwasilisha barua katika shirikisho la soka nchini(Tff) kuhusiana na suala hilo ambapo barua hiyo inasomeka kuwa beki huyo amejitoa kushiriki katika timu ya taifa mpaka afya yake itakapotengemaa.

Beki huyo aliumia mwaka huu katika kambi ya timu ya taifa nchini Afrika ya kusini wakati wakijiandaa na mchezo dhidi ya Lesotho na toka aumie hajarudi fiti mpaka jana aliposhiriki mechi ya kwanza na klabu yake ya Simba katika mchezo dhidi ya Mbeya city.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka