Connect with us

Soka

Kagere Agomea Dili La Ulaya

Kwa mujibu wa meneja wa mchezaji wa klabu ya Simba Meddie Kagere aitwaye Patrick Gakumba ni kwamba mshambuliaji huyo amegomea ofa ya kujiunga na klabu ya Levante Fc ya nchini Hispania.

Meneja huyo raia wa Rwanda alibainisha kwamba klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu nchini Hispania maarufu kama La liga ilimuona Kagere wakati akiitumikia klabu ya Simba katika mchezo dhidi ya klabu ya Sevilla ambapo walionyesha nia ya kumsajili japokua mkataba aliokua nao na Simba sc ndio ulikua kikwazo.

Gakumba amebainisha kwamba hivi sasa staa huyi tayari anahitajika na timu hiyo japokua hawajakubaliana na suala la kufanya majaribio ya miezi sita kama wanavyotaka wahispania hao.

Hata hivyo inasemekana staa huyo mzaliwa wa Burundi mwenye uraia wa Rwanda tayari amekubaliana dau na klabu yake ya Simba na ataongeza mkataba.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka