Connect with us

Soka

Kaduguda Ndani Ya Msimbazi

Klabu ya Simba imemteua Mwina Kaduguda kushika wadhifa wa kaimu Mwenyekiti wa klabu hiyo baada ya Swedi Nkwambi kujiuzulu wadhifa huo miezi kadhaa iliyopita.

Nkwambi ambaye alichaguliwa na wanachama alijiuzulu nafasi hiyo ili kushughulikia masuala yake binafsi kwa mujibu ya barua yake aliyoandika kwa uongozi wa klabu hiyo huku taarifa za ndani zinadai alishindwa kuelewana na baadhi ya viongozi wa bodi ya wakurugenzi ya klabu hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu hiyo Kaduguda atakaimu nafasi ya mwenyekiti ikiwa ni kwa mujibu wa ibara ya 50 ya katiba ya klabu hiyo huku tarehe rasmi ya uchaguzi kujaza nafasi hizo utatangazwa badae.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka