Connect with us

Soka

Kabwili Amwaga Ubuyu

Kipa kinda wa klabu ya Yanga Ramadhani Kabwili amefunguka kuhusu kuzongwa na watu waliojitambulisha kuwa ni viongozi wa Simba sc kutaka kumhonga gari ili asicheze pambano la watani wa jadi la mzunguko wa pili mwaka jana.

Pambano hilo lililoisha kwa Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Meddie Kagere lilimshuhudia Kabwili akikaa langoni baada ya kuwa golikipa namba moja Beno Kakolanya kuingia katika mgogoro  na klabu hiyo.

Kabwili alifunguka kuhusu mkasa huo wa kutaka kuhongwa gari ili apate kadi ya njano itakayomfanya akose pambano hilo ili apangwe golikipa Klause Kindoki ambaye alikua na rekodi mbovu ya kufungwa magoli ya kizembe.

“Mchezo wa kwanza alidaka Beno Kakolanya, mzunguko wa pili tulibaki mimi na Kindoki, nilikuwa na kadi mbili za njano na ilibaki michezo mitatu kucheza na Simba SC , ilikuwa dhidi ya Coastal, Singida na JKT Tanzania. . Nilicheza na kumaliza salama michezo miwili bila kupata kadi dhidi ya Coastal na Singida. . ndipo nikafuatwa na viongozi fulani wa Simba SC wakaniahidi kunipatia gari mpya IST na kwa uhakika zaidi watanisainisha document zote za umiliki wa gari kabla ya mchezo dhidi ya JKT Tanzania ila kwa sharti moja tu nipate kadi ya njano ili mchezo dhidi yao niukose adake Kindoki wakiamini watapata magoli mengi ! sikukubaliana nao na siwezi kufanya hayo, kiukweli nilipata usumbufu mkubwa sana na ni sababu iliyonifanya niache kutumia line ya Tigo ili kuwakwepa”Alifunguka Kabwili.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka