Connect with us

Soka

Juventus Watwaa Ubingwa Serie A

 

Rasmi Juventus ni mabingwa wa Italia wakiwa na mechi mbili mkononi baada ya kuibuka na ushindinwa mabao 2-0 dhidi ya Sampdoria na kufanikiwa kucheza mechi 36 kati ya 38 na kufikisha alama 83 ambazo hazitafikiwa na timu nyingine.

Mabao ya bibi kizee hao yalifungwa na Cristiano Ronaldo pamoja na Bernadeschi na kuwaacha wapinzani wao wanaoshika nafasi ya Pili Inter Milan wenye alama zao 76.

Ronaldo amefikisha goli lake la 31 msimu huu katika ligi nyuma ya kinara Ciro Immobile anayeichezea Lazio Fc mwenye magoli 34.

Juventus wanatwaa ubingwa huo kwa mara ya tisa mfululizo huku usajili wao wa mastaa kama Ronaldo ukionekana kuwalipa zaidi japo wana umri mkubwa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka