Connect with us

Soka

Jang’ombe Boyz Hali Tete

Timu ya Jang’ombe Boys ipo tayari kujitoa Ligi Kuu Zanzibar kutokana na ukata wa fedha, timu hiyo haijaanza hata mazoezi kwa sababu haina fedha za uendeshaji.

Juni 24 ligi kuu ya Zanzibar inatarajiwa kuendelea lakini Jang’ombe Boys wamesema hawawezi kuendelea na ligi hadi hapo watakapowezeshwa.

“Timu yetu inaendeshwa na wafanyabishara ndogondogo ambao walikuwa wanachanga lakini kwa sasa hawafanyi tena biashara. Watu wengine waliokuwa wanatusaidia ni wafanyakazi wa hotelini lakini kwa sasa hoteli nyingi hazifanyi kazi”-Ally Othman Kibichwa, Rais Jang’ombe Boys.

“Tukisema tuwaite wachezaji kwenye mazoezi itabidi wakati wa kuondoka tuwape chochote, sasa hiyo hela sisi tutaitoa wapi?

“Kama hatutawezeshwa hatuwezi kurudi kwenye ligi na uamuzi wowote itakaochukua ZFF sisi tupo tayari. Hatugomi kurudi kwenye ligi lakini hatuna uwezo wa kuendesha timu.”

“Kama hali itaendelea kuwa hivi, sisi watatusamehe na tutakuwa tayari kwa maamuzi yoyote yatakayochukuliwa. Kama tutakosa pesa bora tupumzike tu.”

Jang’ombe Boys ipo kwenye hatari ya kushuka daraja, ipo nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 25 baada ya kucheza mechi 22. Msimu huu timu sita (6) zitashuka daraja (kuanzia nafasi ya 11 hadi 16)

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka