Connect with us

Soka

Inter kileleni,Juve noma Seria A

Ligi kuu nchini Italia(Seria A) imeendelea mwisho mwa juma kwa mechi kali zilizowakutanisha wababe wa ligi hiyo ambapo As Roma ya Mourinho ilwapokea Juventus,huku Inter Milan ikiwaalika Lzio ya Sari Sansiro.

AS Roma wakiwa nyumbani wamepokea kichapo cha 4-3 kutoka kwa Juventus katika moja ya mechi za kusisimua kwenye ligi hiyo msimu huu,mpaka daikika ya 70 Roma walikuwa mbele kwa 3-1 kwa mabo ya Tammy Abraham 11′,Henrikh Mikhtaryan 48′ na Lorenzo Pellegrini 53′.Mbadiliko ya kuingia kwa Arthur Melo yaliimarisha Juve katikati mwa uwanja na kuanza kutawala mchezo.

Dakika ya 70 kiungo Manuel Locatelli aliiandikia Juve goli la pili kabla ya dakika mbili baadae Dejan Kulusevski kufanaya matokeo kuwa 3-3,wakiwa wanajiuliza Roma walishangazwa tena dakika ya 77 kwa bao kutoka kwa Matia De Siglio.Roma wangeweza kusawazisha pale walipopata penati dakika ya 90 lakini nahodha Pellegrini alikosa mkwaju huo.

Inter Milan wameendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya Lazio kwa mabao ya Bastoni na Milan Skriniar huku lile la Lazio likiwekwa kimia ni na Cirlo Immobile.

Atalanta wao walipata ushindi mnono wa 6-2 dhidi ya Udinese kwenye mchezo ulizalisha jumla ya magoli 8.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka