Connect with us

Soka

Hitimana aachana na Simba

Kocha msaidizi wa mabingwa wa tetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba sc Thiery Hitimana ameachana na klabu hiyo baada ya kusitishwa kwa mkataba wake na waajiri wake hao.

Mrwanda huyo alijiunga na Simba zaidi ya miezi mitatu iliyopita ili kusimamia benchi la ufundi la timu hiyo kwenye michuano ya kombe la klabu bingwa Afrika kutokana makocha Didier Gomez wa wakati huo na msaidizi wake Suleiman Matola kukosa sifa na vigezo kwa mujibu wa kanuni za CAF.

Hapo awali aliicha njiani klabu ya Mtibwa sugar ambayo ndiyo iliyomleta kukinoa kikosi chao lakini ofa ya Msimbazi ilimvutia zaidi kiasi cha kukubali kuwa kocha msaidizi licha ya kuwa na vigezo vyote vya kuwa kocha mkuu.

Taarifa rasmi ya klabu ya Simba kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa klabu hiyo ni kama ifuatavyo

Hata hivyo huenda kocha huyo akajiunga na Mtibwa sugar ambayo inatafuta kocha mpya mkuu baada ya kumfuta kazi Mcameroon Joseph Omog hivi karibuni.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka