Soka
HII SASA KAZI, AJIBU ATAKIWA NA BOSS WAKE KUTAJA SABABU ZINGINE ZA KUIKACHA TP MAZEMBE
Kocha Mkuu wa Yanga Mkongomani, Mwinyi Zahera amesema kuwa kiungo wake mshambuliaji, Ibrahim Ajibu atafute sababu nyingine iliyomzuia kujiunga TP Mazembe ya DR Congo na siyo dau la usajili.
Kauli hiyo aliitoa ikiwa ni siku chache ziibuke taarifa za dili la Ajibu kushindikana kwa kile kilichoelezwa kushindwana katika dau la usajili ambalo Mazembe walitenga dola 30,000 (zaidi ya Shilingi Milioni 60).
Mara ya taarifa hizo kuzagaa za kushindikana kutua Mazembe zikaibuka tetesi za nyota huyo kwenda Simba baada ya kusaini mkataba wa awali wa miaka miwili huku akitanguliziwa Shilingi Milioni 20.
Zahera alisema ni ngumu kwa Mazembe kushindwana na Ajibu katika dau la usajili.
“Ninaahidi kufuatilia kwa ukaribu usajili wake na kikubwa kujua dau la usajili alilowekewa mezani na klabu hiyo.”
“Mimi ndiye niliyefanikisha mipango hiyo ya Ajibu kusaini Mazembe, kwani nilimwambia kocha wa Mazembe amenipigia simu kaniulizia kuhusu wewe na uzuri nilimpa taarifa zako zote nzuri nikamuuliza upo tayari kujiu..