Connect with us

Soka

Hakuna Ubishi

Hakuna tena ubishi mtaani baada ya Simba sc kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Yanga sc katika mchezo wa hatua ya nusu fainali kombe la shirikisho la Azam mchezo uliofanyika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Mabao ya Simba iliyo chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck yalipatokana katika  ushindi huo kupitia kwa Gerson Fraga dakika 21, Clatous Chama dakika ya 50, Luis Miqussone dakika ya 52 na Mzamiru Yassin dakika 88.

Yanga sc walipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Feisal Salum dakika ya 70 baada ya kupiga kiki iliyomshinda Aishi Manula na kutoa matumaini kwa Yanga sc.

Simba sasa itacheza na Namungo Fc mchezo wa fainali ya kombe hilo utakaofanyika mjini Sumbawanga mkoani Rukwa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka