Rais mpya wa Klabu ya AS Vita, mwanamama mrembo, Bestine Kazadi, ameweka wazi kuwa kocha wa mkuu wa timu hiyo, Frolent Ibenge hawezi kwenda popote ikiwa ni siku chache tu baada ya kuwepo kwa taarifa za kutakiwa na mabingwa wa Ligi Kuu Bara, Simba.
Kocha huyo mwenye uwezo mkubwa katika soka la kimataifa, amekuwa akihusishwa na Simba mara kwa mara huku mwenyewe akiri kuwa yupo tayari kujiunga na timu hiyo ikiwa atapewa ofa nzuri.
Hivi karibuni, redio ya kimataifa ya Ufaransa ilimuhoji rais huyo ambaye ni mwanamke wa kwanza Afrika kuongoza klabu kubwa, ambapo alisema Ibenge ataendelea kubaki hapo kwa kuwa bado wana mipango naye mingi.
“Mashabiki wajue kuwa Ibenge atabaki kuendelea kuwepo kwenye klabu yetu kama mkuu wa benchi la ufundi, waachane na hayo wanayosikia, hawezi kwenda popote.
“Wanapaswa kujua kwamba atabaki kuwa na sisi kwanuna mipango naye mingi ikiwemo ya kuhakiki-sha tuna-wa Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja kuendelea kuifanya timu yetu ya AS Vita iwe timu kubwa kibiashara na hata huko mnaposikia hawezi kwenda,” alisema Kazadi.
Ibenge alijiunga na timu hiyo mwishoni mwa mwaka 2012 na amefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Congo mara mbili, huku akichukua medali za mshindi wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika.
Cc:Mitandao/jamilakassim