Connect with us

Soka

Gwambina Wairejesha Yanga Usiku

Baada ya kulazimishwa matokeo ya suluhu dhidi ya Coastal Union jana, kikosi cha Yanga kilisafiri usiku kwa usiku kurejea jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo wa kombe la FA dhidi ya Gwambina FC

Mchezo huo utapigwa kweshokutwa Jumatano Februari 26 kwenye uwanja wa Taifa ambapo Yanga inatakiwa ishinde ili kuendelea na hatua inayofuatia.

Kutokana na mwenendo wa kusuasua kwenye ligi, Yanga italazimika ‘kukomaa’ na FA ili kuhakikisha inatwaa taji hilo kupata nafasi ya kushiriki michuano ya Shirikisho barani Afrika msimu ujao Kwani Matumiani ya kutwaa taji la ligi kuu tayari yametoweka.

Baada ya kutoka suluhu hapo jana ili Yanga iwe bingwa wa ligi kuu inatakiwa ishinde mechi zake zote zilizosalia huku Simba ipoteze mechi sita kati ya 14 ilizobakiza.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka