Connect with us

Soka

Gsm Yamrejesha Lamine

Kampuni ya Gsm imefanikiwa kumrejesha beki wa klabu ya Yanga sc Lamine Moro baada ya kusaidia mazungumzo ya kumaliza matatizo baina ya mchezaji huyo na klabu hiyo.

Lamine aliondoka Jangwani baada ya kuandika barua ya kuvunja mkataba kufuatia kucheleweshewa baadhi ya stahiki zake ikiwemo mishahara na posho hivyo kuamua kuvunja mkataba na klabu hiyo.

Hata hivyo licha ya kuonyesha nia ya kuvunja mkataba huo klabu hiyo ilijitahidi kumrejesha mchezaji huyo hasa baada ya kupata tetesi za kukaribia kujiunga na Simba mpaka walipofanikiwa baada ya kampuni ya Gsm kuingilia kati kumaliza tatizo hilo.

Lamine tayari amerejea nchini na tayari amemalizana na uongozi wa klabu hiyo huku akithibitisha kuendelea kutumikia mkataba wake na klabu hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka