Connect with us

Soka

Gsm Waipiga Chini Yanga

Wadhamini wa klabu ya Yanga kampuni ya Gsm wamejitoa kuisaidia timu katika baadhi ya vitu ambavyo havimo katika mkataba kama kusaidia usajili pamoja na kulipa mishahara ya wachezaji na makocha wa klabu hiyo.

Katika barua iliyoandikwa na kampuni hiyo kwenda kwa mwenyekiti wa klabu ya Yanga Mshindo Msolla imeanisha sababu ya kusimamisha misaada hiyo  ni baada ya baadhi ya wajumbe wa klabu hiyo kulalamika kuwa kampuni hiyo inaingilia shughuli za utawala za klabu hiyo.

Pia kampuni hiyo imeanisha kuwa haitahusika na kulipa bonusi zote ilizokua inatoa pamoja na kulipia huduma za kambi kama ilivyokua awali badala yake watajikita katika zaidi katika mauzo ya jezi za klabu hiyo kama mkataba unavyosema.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka