Connect with us

Soka

Gsm Wainogesha Yanga

Kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Coastal union wachezaji wa Yanga wamepata zawadi wa shilingi milioni kumi kutoka kwa wadhamini na wasambazaji wa jezi za timu hiyo kampuni ya Gsm fedha ambazo zitatolewa katika kila mechi ambayo watashinda.

Gsm inayomilikiwa na tajiri Gharib Said Mohamed ambayo imedhamini Yanga kupitia godoro la Gsm Foam na huku wakilamba dili la usambazaji wa jezi za klabu hiyo kupitia maduka mbalimbali(Malls) yanayomilikiwa na kampuni hiyo imeamua kujitolea kiasi hicho cha fedha katika kila mechi ambayo timu hiyo itashinda na ambapo tayari kiasi hicho cha fedha kimekabidhiwa kwa wachezaji kufuatia ushindi huo.

Juma Abdul ambaye alikua nahodha kwenye mchezo huo kufuatia kutokuwepo kwa nahodha mkuu Papy Kabamba Tshitshimbi ambaye anasumbuliwa na majeraha tayari amethibitisha wachezaji kupokea kiasi hicho cha fedha.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka