Connect with us

Soka

Goti Lamtibulia Beki Yanga

Maumivu ya goti aliyoyapata beki wa Yanga Ally Ally yamemfanya atolewe kwenye kikosi cha timu hiyo kitakachovaana na Township Rollers jijini Gaborone Botswana.

Beki huyo mfupi mwenye uimara katika kucheza mipira ya juu alisajiliwa na Yanga akitokea Kmc ya jijini Dar es salaam na amefanikiwa kupata nafasi katika baadhi ya michezo ukiwemo dhidi ya Rollers alipoingia kuchukua nafasi ya Paulo Godfrey ambaye alipata majeraha.

Beki huyo alikuwemo kwenye msafara wa wachezaji waliosafiri kwenda nchini humo japo kutokana na maumivu hayo kuna uwezekano wa kutocheza mchezo huo.a

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka