KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems raia wa Ubelgiji, amefunguka kwamba kwa sasa anapiga hesabu za kukisuka upya kikosi chake na kwenye usajili wa msimu ujao ambapo amepanga kuongeza sura mpya tatu ndani ya kikosi chake.
Mbelgiji huyo amesema sura hizo ambazo zitaonekana kwenye kikosi chake nia kwenye eneo la ulinzi, kiungo na ushambuliaji. Kocha huyo ametaka kufanya usajili kwenye maeneo hayoa baada ya kuona wingi wa makombe ambayo watacheza Simba msimu ujao.
Simba kwa msimu ujao watashiriki Ligi ya Mabingwa Afria baada ya kuwa mabingwa wa ligi, Kombe la Mapinduzi, Kombe la Shirikisho (FA), SportPesa Super Cup na Ligi Kuu Bara.
Aussems ameliambia Championi Jumatano, kuwa ataongeza idadi ya wachezaji hao kutokana na kutaka kuwa na kikosi kipana zaidi na watu ambao watafanya kazi kuhakikisha timu inafanya vizuri zaidi ya msimu huu.
“Hesabu zangu kwa sasa ni namna ambavyo tuna kazi kubwa ya kutetea ubingwa kwa msimu ujao sambamba na maatajia mengine ambayo tutashiriki. Kwa kuliona hilo ninataka kufanya usajili wa aina yake ili kuongeza upana wa timu.
“Nafikiria kwenye usajili huu kuongeza wachezaji katika sehemu za ulinzi ambapo ninahitaji mwenye uzoefu zaidi wa michuano ya kimataifa, kiungo mmoja na mshambuliaji mwenye auwezo wa juu wa kufunga mabao ambaye atakuja kufanya kazi na kina Bocco (John), Kagere (Meddie) na Okwi (Emmanuel) katika eneo hilo.
“Ninafanya hivyo kwa sababua ya malengo makubwa ambayo tumeyaweka, tunahitaji kufi ka mbali zaidi kwenye Ligi ya Mabingwa zaidi ya robo fainali tulipofi ka, kutetea ubingwa wa ligi kama ilivyo msimu huu lakini kuchukua matajia mengine ambayoa msimu huu imekuwa ngumu kuyachukua,” alisema Aussems ambaye atasajili akiwa kwao.
“Baada ya ligi kuisha (iliisha jana Jumanne) nitaondoka kwenda nyumbani kupumzika, kwa sababu nimemaliza kazi ya msimu huu, lakini nitaenda kujiandaa na msimu ujao ambao ninatakiwa kufanya vizuri zaidi ya msimu huu.
“Nikiwa huko nitaacha ripoti ya usajili kwa viongozi juu ya nani ambaye ninahitaji awemo ndani ya kikosi changu kwa msimu ujao na kina nani ambao wasiwepo, nitakaporudi hapa nchini itakuwa ni kazi moja tu kuanza kukisuka kikosi kwa ajili ya msimu ujao,” alisema Aussems.\
CHANZO: CHAMPIONI