Connect with us

Soka

Fifa Kuishushia Rungu Uganda

Shirikisho la Kandanda Duniani (FIFA) limetoa onyo kwa nchi ya Uganda kuwa litaifungia kujihusisha na masuala ya soka ikiwa serikali ya nchi hiyo itaingilia masuala ya soka. Onyo hilo limetolewa ikiwa ni siku chache baada ya serikali ya Uganda kutangaza nia ya kufanya uchunguzi juu ya tuhuma za ubadhilifu wa fedha zinazomkabili Rais wa Shirikisho la Soka la Uganda (FUFA) Injinia Moses Magogo.
Magogo anadaiwa kuhusika na mauzo ya tiketi za kutazama Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 zilizofanyika nchini Brazil ambazo FUFA ilipatiwa na FIFA jambo lililofanya shirikisho hilo la soka ulimwenguni kuanzisha uchunguzi uliomtia hatiani na kupelekea kupewa adhabu ya kufungiwa kujihusisha na soka kwa muda wa miezi miwili sambamba na faini ya kiasi cha fedha kiasi cha Faranga za Uswizi 10,000 (Sh 37 milioni za Uganda ), Lakini pamoja na adhabu hiyo ya FIFA.
Barua iliyoandikwa na Katibu Mkuu wa FIFA, Fatma Samoura imeitaka Uganda kuachana na mpango huo vinginevyo itakutana na rungu la kufungiwa.
“Ni jukumu letu kulijulisha Shirikisho la Soka Uganda (FUFA) kuwa vitendo vyovyote ambavyo vitapelekea uvunjaji wa Ibara ya 14 kifungu cha 1 (i) utapelekea adhabu hadi ya kusimamishwa kwa FUFA. Na kusimamishwa kwa FUFA kutasababisha moja kwa moja kusimamishwa kwa fedha za mradi wa FIFA Forward na ushiriki wa timu za taifa za Uganda na klabu zake kwenye mashindano ya kimataifa,” ilifafanua barua hiyo ya Samoura.

Credit:Dominick Salamba

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka