Connect with us

Soka

Ferguson Aibusti Psg

Kocha wa zamani wa Klabu ya Manchester United, Sir Alex Ferguson, siku ya leo alienda kukutana na Raisi wa Klabu ya PSG, Nasser Al-Khelaifi, katika hotel Lowry waliyofikia Klabu hiyo Jijini Manchester.
Ikumbukwe siku ya leo Klabu ya PSG itacheza mchezo wa mkondo wa pili wa hatua ya Nusu fainali ya UEFA Champions League dhidi ya Manchester City utakaopigwa Etihad kuanzia saa 22:00 Usiku.
Fergie anasadikika kuwa hasimu mkubwa wa klabu ya Manchester City ambayo imechukua ufalme wa jiji la Manchester huku pia wakielekea kuchukua taji la ligi kuu nchini humo.
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Nchini Ufaransa Jijini Paris, Klabu ya Manchester City iliibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Wenyeji wao PSG.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka