Connect with us

Soka

Epl Yaleta Kizungumkuti

Bodi ya Ligi kuu England imetoa pendekezo la kucheza michezo ya Premier League bila mashabiki kuanzia May 02 Hadi July 12 mwaka huu. Pendekezo hilo litajadiliwa na vilabu vyote 20 Ijumaa hii kwa njia ya Mtandano na wadau Kama serikali, mamlaka za afya na chama cha wachezaji wa kulipwa (PFA).

Lengo la Bodi kuirejesha EPL ni kukwepa hasara kubwa ya kifedha kama msimu hautamalizika kwasababu ya mlipuko wa virusi vya Corona. Kinachowaumiza zaidi Bodi ni mkataba wa mwaka mmoja wa haki za matangazo wenye thamani ya Pauni bilioni tatu, unaopaswa kumalizika Julai 31.

Kama msimu hautamalizika hivi Sky Sports, BT Sport na kampuni nyingine za kimataifa zenye haki ya kurusha Live Premier League zitatakiwa kufidiwa kwa pamoja, jumla ya pauni Milioni 762.Tayari wenye haki za matangazo, wameanza kuipa presha Bodi, wakitaka kujua ni lini EPL itarejea kwasababu wanazidi kupoteza wateja wa kulipia.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka