Connect with us

Soka

Epl kuendelea Boxing day

Ligi kuu soka nchin Uingereza itaendelea tena leo Jumapili ya Boxing day kwa mechi takribani sita baada ya kupisha sikukuu ya Christmas kusaka alama muhimu kwenye jedwali la msimamo wa ligi.

Mechi tatui zilizokuwa zichzwa hii leo zimeahirishwa kutokana na muendelezo wa maambukizi ya Uviko-19 kwa wafanayakazi na wachezaji wa vilabu vya ligi hiyo.Mechi hizo ni ile ya kati ya Burnley dhidi ya Everon pamoja na ile ya Liverpool dhidi ya Leeds United.Mwingine ni ule wa Wolves dhidi ya Watford

Katika vita ya kuwania ubingwa kutakuwa na mechi mbili kati ambazo ni Manchester city watakaokuwa Etihad kuwakaribisha Leicester city huku Chelsea watasafiri hadi Villa Park kuwavaa Aston Villa waliokwenye kiwango bora siku za hivi karibuni baada ya ujio wa kocha Steven Gerrard.

Hata hivyo Gerrard ataukosa mchezo wa leo kutokana na kupata Uviko-19,washika bunduku kutoka London Arsenal walikwenye kiwango bora tangu kuingia kwa Disemba hii watakuwa Carrow roads kucheza na Norwich city.

Mechi nyingine za leo ni;

West Ham United vs Southampton (saa 12 jioni)

Tottenham Hotspur vs Crystal Palace (saaa 12 jioni)

Brighton vs Brentford (saa 5 usiku)

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka