Connect with us

Soka

Enrique Arejea Spain

Luis Enrique ameteuliwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Hispania baada ya hapo awali kujiengua kutokana na matatizo ya kiafya ya mwanaye wa kike.

Kocha huyo wa zamani wa Barcelona alijiuzulu mwezi june mwaka huu kutokana na afya ya mwanaye kutetereka baada ya kuugua kansa na baadaye alipoteza maisha mwezi septemba huku nafasi yake timu ya taifa ikichukuliwa na Roberto Moreno.

Erique atakua na kazi ya kuiandaa timu ili kufuzu michuano ya ulaya ya mwaka 2020 huku uzoefu wa kuinoa Barcelona kwa misimu mitatu ikitajwa kuwa chachu ya kupewa nafasi hiyo.

Kabla ya nafasi hiyo Erique alikua anahusishwa kutua klabu ya Arsenal kuchukua nafasi ya Unai Emiry ambaye nafasi yake ipo matatani kufuatia mfululizo wa matokeo yasiyoridhisha

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka