Connect with us

Soka

Dybala Kutolewa Chambo Kisa Neymar

Timu ya Juventus imetuma ofa ya mshambuliaji Paulo Dybala na kiasi cha fedha kwenda Psg ili kumnasa mshambuliaji Neymar ambaye ameonesha nia ya kuondoka jijini Paris huku Barcelona na Real Madrid zikitajwa ndio chaguo la staa huyo.

Juve wanataka kumtoa Dybala ambaye kocha Mauricio Sarri amethibitisha kuwa hayupo katika mipango yake bali timu nzima itaundwa kumzunguka Cristiano Ronaldo.

Awali juve ilitaka kumuuza staa huyo kwenda Manchester United kwa fedha kamili ama kwa mabadilishano na Romelu Lukaku lakini dili hilo lilishindikana baada ya wakala wa staa huyo kudai mshahara mkubwa na dau la wakala kuwa kubwa hivyo united wakabadili uamuzi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka