Connect with us

Soka

Dybala Anukia Man utd

Timu za manchester united na Juventus zipo katika mazunguzo ya kubadilishana wachezaji Romelu Lukaku na Paulo Dybala ili kuboresha vikosi vyao kwa msimu ujao.

Lukaku amekosa nafasi katika kikosi cha Ole Gunnar Solskjaer na hivi karibuni aliachwa katika msafara wa kikosi hicho kilichokwenda Norway katika mchezo wa kirafiki ambao united ilishinda kwa goli moja lililofungwa na Juan Mata.

Inadaiwa Solskjaer ni muumini wa washambuliaji wanaonyumbulika ndio maana anampa nafasi Athony Martial mbele ya Lukaku huku akiona ongezeko la Dyballa lina faida ya kuongeza makali kikosini hapo pia unyambulifu wa mchezaji huyo akiwa na uwezo wa kucheza nafasi zote za mbele.

Juve wanahitaji fedha kiasi na Lukaku huku wakimthaminisha mchezaji huyo kwa dau la paundi milioni 100 hivyo kulingana na thamani ya Lukaku ya paundi milioni 75 united itawalazimu kuongeza katika ya paundi milioni 10-20 ili kukamilisha dili hilo.

Inadaiwa wakala wa Dyabala ameshatua London kwenye ofisi ndogo ya Mashetani wekundu ili kukubaliana maslahi binafsi na mabingwa hao mara 13 wa ligi kuu ya Uingereza.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka