Connect with us

Soka

Dante,Yanga Bado Utata

Beki wa klabu ya Yanga sc Andrew Vicent “Dante” amegoma kujiunga na timu hiyo akishinikiza kulipwa fedha za usajili anazoidai timu hiyo.

Beki huyo aliyejiunga na timu hiyo akitokea Mtibwa sugar amejiondoa katika timu hiyo akishinikiza alipwe madai hayo ya fedha za usajili za miaka miwili iliyopita ambapo inasemekana fedha hizo zinakaribia shilingi milioni 45.

Kocha Mwinyi Zahera alisisitiza madai ya beki huyo kushughulikiwa baada ya kujitoa kwa msimu uliopita kuipambania timu hiyo ilipokua na hali ngumu kiuchumi.

“Milango iko wazi kurejea kama anaweza kukubali  kulipwa kidogo kidogo”alisema makamu mwenyekiti wa klabu hiyo David Mwakalebela.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka