Connect with us

Soka

Dante Aigomea Yanga

Beki wa klabu ya Yanga Andrew Vicent “Dante” ameiwekea ngumu klabu hiyo kumlipa fedha zake kwa awamu kama inavyofanya kwa mastaa wengine huku akihitaji kulipwa zote kwa mkupuo mmoja.

Staa huyo anaidai timu hiyo kiasi cha shilingi milioni 40 ikiwa ni fedha za usajili pamoja na mishahara ameombwa na klabu hiyo kukubali kulipwa kwa awamu tatu ambapo awamu mbili atalipwa milioni 15 na awamu ya mwisho atalipwa milioni 10.

Kwa mujibu wa Afisa Habari wa klabu hiyo Michael Bumbuli  staa huyo amegoma akihitaji kulipwa fedha zote kwa mkupua mmoja tofauti na ilivyokua kwa mastaa wengine akiwemo Juma Abdul ambaye amejiunga na timu hiyo baada ya kukubali kulipwa kidogo kidogo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka