Connect with us

Soka

Corona Yaishtua Caf

Shirikisho la soka barani Afrika-CAF kesho na keshokutwa(Machi 14 na 15,2020) Litaitembelea Cameroon ambao ni Mwenyeji wa mashindano ya wachezaji wanaocheza ligi za ndani barani Africa-CHAN.

Pamoja na mambo mengine shirikisho hilo litaangalia namna Cameroon ilivyojipanga kupambana na virusi hatari vya Corona ambavyo vimekuwa tishio katika mataifa mengine ulimwenguni pia kufanya tathmini kama mashindano hayo yafanyike au la.

Kwa mujibu wa shirika la Afya duniani-WHO,Mpaka sasa nchi 17 barani Afrika zimethibitisha kuwa na visa 160 vya virusi vya ugonjwa wa CORONA tangu ugonjwa huo ulipuke mwishoni mwa mwaka jana nchini CHINA mojawapo ikiwemo Cameroon ikiwa na visa viwili

Mashindano ya CHAN yamepangwa kuafnyika kuanzia Aprili 4-25,2020 ambapo Tanzania ni moja ya timu zilizofuzu kushiriki michuano hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka