Connect with us

Soka

Cecafa Wanawake Yanoga

Timu mbalimbali zimeanza kuwasili Tanzania kuelekea kwenye mashindano ya Cecafa kwa Wanawake yatakayoanza Novemba 16-25,2019 Dar es Salaam.

Tayari timu za Burundi na Djibout zimetua jana Jumanne na kuelekea kwenye Hoteli zilizopangiwa.

Leo timu za Kenya na Ethiopia zinataraji kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Uganda wenyewe wanatarajia kuingia Kesho mchana sawa na Zanzibar huku pia tukiitarajia timu ya Sudan Kusini.

Wenyeji Tanzania Bara “Kilimanjaro Queens” mabingwa watetezi tayari wapo Kambini wakiendelea kujifua.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka