Connect with us

Soka

Cavani,Van De Beek kusalia Utd

Kocha wa muda wa Manchester united Ralf Rngnick ameweka  wazi kuwa mshambuliaji Edson Cavani na kiungo Don Van De Beek wataendelea kubakia ndani ya klabu hiyo hadi mwisho wa msimu huu.

Cavani na Donny wamekuwa wakihusishwa na kuondoka Old Trafford kutokana na kutokupata nafasi za kutosha kucheza kikosi cha kwanza mara kwa mara,licha ya kuwa na uwezo mkubwa kuweza kuanza na kuisaidia timu hiyo kupata matokeo mazuri uwanjani.

Edi amekuwa akitajwa sana Fc Barcelona baada ya kocha wa timu hiyo Xavi Hernandez kutaka kumsajili ili aongeze nguvu idara ya  ushambuliaji ambayo imekuwa ikisuasua,Van De Beek yeye amekuwa akitaka kuondoka ili akapate nafasi ya kucheza,kusudu aitwe kuitumikia timu yake ya taifa ya Uholanzi katika michuano ijayo ya kombe la dunia nchini Qatar baadae mwaka huu.

Katika mahojiano na waandishi wa habari Ralf amesema kuwa ”najua kuna wachezaji wanataka kuondoka,ila nimeongea nao na kuwaambia kuwa tunawahitaji na tutahakikisha wanapata nafasi ya kucheza kwani bado tupo kwenye mashindano matatu,kuhudu Donny niliongea nae wiki iliyopita na najua anataka kurudi kucheza timu ya taifa,na Cavani ni mchezaji muhimu sana na anajua hilo”.

Nafasi za wachezaji hao kuanza kikosini zimekuwa finyu kuyokana na uwepo wa Wareno waili katika nafasi zao,Bruno Fernandes na Cristiano Ronaldo ambao wamekuwa wachezaji muhimu na vipenzi vya mashabiki.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka