Connect with us

Soka

Carlinhos Hatihati Kuwavaa Simba sc

Staa wa Yanga sc Carlos Carlinhos ana uwezekano mkubwa wa kuikosa mechi baina ya watani wa jadi Yang sc dhidi ya Simba sc katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara utakaofanyika katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es salaam siku ya jumamosi Novemba 7.

Staa huyo aliumia katika mazoezi ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Polisi Tanzania ambao Yanga sc iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Mukoko Tonombe.

Kwa mujibu wa ripoti za ndani Carlinhos alishaanza mazoezi lakini anakosa utimamu wa mwili kuweza kushiriki mchezo huo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka