Connect with us

Soka

Buswita Atua Polisi

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Mbao Fc na Yanga sc Pius Buswita amejiunga na timu ya Polisi Tanzania baada ya kuwa nje kwa nusu msimu tangu atemwe na Yanga.

Mchezaji huyo mwenye uwezo wa kucheza kiungo wa kati na pembeni amejiunga na timu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja katika usajili wa dirisha dogo linalofunguliwa kuanzia disemba 15 mwaka huu.

Buswita alisajiliwa na Yanga baada ya kufanya vizuri misimu miwili iliyopita akiwa katika klabu ya Mbao fc ambapo alikua na uhakika wa namba enzi za kocha George Lwandamina kabla ya kuja kocha Mwinyi Zahera ambae alimtema.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka