Connect with us

Soka

Bundasliga Waanza Mazoezi

Vilabu vya ligi kuu nchini Ujerumani Bundasliga vimeruhusiwa kuanza mazoezi huku vikichukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Covid-19 wakati ligi zote nchini humo zikiendelea kusimama hadi baada ya Aprili 30, 2020 itakapotangazwa vinginevyo.

Mabingwa watetezi, Bayern Munich wamekuwa wa kwanza kufurahia ruhusa hiyo na wamesema wataanza vipindi vyao vya mazoezi mara moja huku baadhi ya timu zikisema zitafanya mazoezi yao kwa makundi badala ya wachezaji wote kukutana sehemu moja.

Nchi mbalimbali duniani zimesimamisha shughuli zote za michezi ili kuepuka mkusanyiko ya watu ikiwa ni njia ya kudhibiti Virusi vya Corona.

Cc:Azam tv.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka