Connect with us

Soka

Bruno Atua Man Utd

Hatimaye tetesi za muda mrefu kuhusu usajili wa kiungo Bruno Fernandes kutoka Sporting Lisbon kwenda Man United zimefika kikomo baada ya dili hilo kukamilika rasmi.

Sporting wamethibitisha taarifa za kumuuza kiungo wao Fernandes kwa kiasi cha £68m huku Man United wakilipa kiasi cha £46.6m kama malipo ya awali na zingine zitalipwa kama malipo ya nyongeza kutokana na vipengele mbalimbali.

Sporting watapata £4.2m endapo Man United watafanikiwa kupata nafasi ya kushiriki ligi ya mabingwa Ulaya msimu ujao.

Man United pia watalipa kiasi cha £12.6 endapo Fernandes atafanikiwa kuchukua tuzo binafsi na wakala wake pia atapokea £4.6m.

Sporting pia wameeleza kuwa wameweka kipengele cha kupata asilimia (10%) endapo Man United watamuuza Fernandes.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka