Connect with us

Soka

Beki Matata Kutua Simba sc

Klabu ya Simba imeanza mazungumzo na Beki wa Kati wa klabu ya Dynamos ya Zimbabwe na timu ya taifa ya Zimbabwe Patson Jaure mwenye umri wa miaka 30.

Simba wanamtaka beki huyo mwenye uzoefu ikiwa ni mlakati wa kuimarisha Kikosi chao hasa katika safu ya Ulinzi kwa ajili ya michuano ya Klabu bingwa Africa na ligi kuu Tanzania bara.

Kazi ya kumpata beki huyo inaweza isiwe ngumu kwa Simba SC Tanzania kwani wanaweza kumtumia kocha wao wa zamani Zdvradko Logarusic ambaye ndiye anayekinoa Kikosi cha timu ya Taifa ya Zimbabwe kitakachoshiriki fainali zijazo za CHAN,

Kama hiyo haitoshi Simba bado wanaweza kumtumia Kiungo wao wa zamani Justice Majabvi kumshawishi beki huyo kujiunga na mabingwa hao wa Vodacom Premier league.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka