Connect with us

Soka

Beki Lipuli Kutua Simba sc

Mabingwa mara tatu mfululizo wa VPL, Simba SC wamefikia hatua nzuri ya kumsajili beki wa kulia wa Lipuli, David Kameta kwa mkataba wa miaka miwili.

Msimu huu Kameta ameifungia Lipuli magoli mawili na asisti sita, akionyeshwa kadi sita za njano na moja nyekundu huku akitarajiwa kwenda msimbazi kuwa mbadala wa Shomari Kapombe anayesumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara.

Hivi karibuni Afisa Mtendaji mkuu wa klabu ya Simba sc Senzo Mbatha Mazingisa alisikika akisema kuwa klabu hiyo ina mpango wa kusajili wachezaji wachache wenye tija huku ikitema mastaa wasiopungua watano.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka