Connect with us

Soka

Bei Ya Makambo Yaleta Taharuki

Mashabiki wa soka nchini wamepigwa na taharuki kuhusu bei halisi aliyouzwa aliyekua mshambuliaji wa klabu ya Yanga Heritier Makambo baada ya aliyekuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo kutoa siri nzito.

Mjumbu huyo anayefahamika kwa jina la Shija Richard amebainisha ya kwamba awali waliambiwa kuwa staa huyo anahitajika kwa kiasi cha shilingi milioni 170 za kitanzania ambapo walikubaliana na dau hilo kutokana na timu kuhitaji kufanya usajili lakini baadae waligundua kuwa mchezaji huyo aliuzwa kwa fedha nyingi zaidi.

Shija anasema walijadiliana kama kamati ya utendaji na kukubaliana kuhusu suala hilo lakini baadae waligundua kuwa staa huyo aliuzwa kwa dau la milioni 250 huku kocha Mwinyi Zahera akiwa ndio wakala wa mchezaji huyo.

Kufuatia kauli hizo za aliyekua mjumbe wa kamati ya fedha ya klabu hiyo baadhi ya wadau wamekua na taharuki huku wakitoa maoni mbalimbali kuhusu suala hilo la Zahera kuweka udalali katika biashara ya mchezaji huyo huku baadhi ya wapenzi wa klabu ya Simba wakiwacheka wale wa Yanga kuwa wameingizwa mjini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka