Connect with us

Soka

Bayern Yakomaa na Guardiola

Klabu ya soka ya Bayern Munchen inayoshiriki ligi kuu nchini ujerumani inataka kumrudisha kocha Pep Guardiola wa Manchester city kuifundisha klabu hiyo baada ya kuachana nae miaka kadhaa iliyopita.

Bayern ilipitia katika wakati mgumu katika ligi kuu ya Bundesliga kiasi cha kumtimua kocha Niko Kovac baada ya mfululizo wa matokeo yasiyorodhisha klabuni hapo na mpaka sasa inaangalia makocha wa kuziba nafasi hiyo ambayo wamempa kipaumbele kocha huyo wa Man city.

Kwa sasa Guardiola bado ana mkataba na mabosi zake wanaoutumia Uwanja wa Etihad mpaka 2021 licha ya Bayern Munich kuamini kwamba wanaweza kumshawishi kurejea Allianz Arena msimu ujao baada ya miaka minne kupita.

Uwezekano wa Bayern kumnasa kocha huyo ni mkubwa ukizingatia mke wa kocha huyo bado anaishi jijini Munich baada ya kugoma kuhamia Manchester tangu awali.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka