Connect with us

Soka

Bayern Yaifanyia Mauaji Totts

Timu ya Bayern Munchen imeifunga Tottenham mabao 7-2 katika mchezo wa kundi B michuano ya klabu bingwa barani ulaya mchezo uliofanyika katika uwanja wa nyumbani wa Tottenham Arena jijini London Uingereza.

Kipigo hicho ni muendelezo wa matokeo mabaya kwa timu hiyo ambayo yanazidi kumuweka matatani kocha Maurico Pochetino baada ya siku za karibuni kuripotiwa kutokuwepo kwa utulivu katika vyumba vya kubadilishia nguo vya timu hiyo.

Serge Gnabry ndio alikua mwiba kwa timu hiyo baada ya kufunga mabao manne katika dakika za 52’55’83’ na 88′ huku mabao mengine yakiwekwa kimiani na mkongwe Robert Lewandowski dakika za 45′ na 88′ huku Joshua Kimmich akisawazisha dakika ya 15′ bao la mapema la Son Heuang Min la dakika ya 12′.

Harry Kane aliwafungia pia Tottenham kwa penati dakika ya 61′ baada ya Kingsley Coman kumchezea faulo Danny Rose na mwamuzi Clement Turpin kutoa penati iliyofungwa na Kane.

“Ni ngumu kuamini aina hii ya matokeo,kila mpira waliopiga uliingia golini kwa kweli imetuangusha sana tunahitaji kuwa imara bayern walikua vizuri lazima tuendelee na mambo mengine”Alisema kocha huyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka