Connect with us

Soka

Barca Waipisha Madrid Kileleni

Klabu ya Barcelona imeshushwa katika msimamo wa ligi kuu nchini Hispania baada ya jana kushindwa kuibuka na ushindi dhidi ya Atletico Madrid baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2.

Barca walifaidika na kitendo cha kutokua makini kwa Diego Costa ambaye alijifunga dakika ya 11 japo makosa yake yalifutwa na Saul Niguez aliyefunga kwa penati dakika ya 19 huku Messi akifanikiwa kufunga bao la pili kwa Barca na la 700 kwake katika michuano yote dakika ya 50 japo nalo halikudumu ambapo Saul Niguez alifunga penati ya pili dakika ya 62.

Kwa matokeo hayo Real Madrid wameendelea kusalia kileleni licha ya kuwa na mchezo mmoja mkononi wakiwa na pointi 71 huku Barca wakiwa na pointi 70 katika nafasi ya pili.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka