Connect with us

Soka

Banka Arejeshwa Yanga

Joto la pambano la watani wa jadi limezidi kuchukua sura mpya kufuatia kuambatana na matukio lukuki kabla ya pambano hilo litakalofanyika julai 12.

Katika kuhakikisha inaibuka na ushindi katika mchezo huo wa nusu fainali kombe la shirikisho klabu ya Yanga sc imemrudisha kundini kiungo Mohamed Issa”Mo banka” ambaye alikua amegoma kujiunga na timu hiyo kushnikiza kulipwa stahiki zake za usajili.

Kiungo huyo ambaye alikua na mchango mkubwa katika pambano walilotoka sare raundi ya kwanza baada ya kusababisha goli la pili baada ya kumghasi Mohamed Hussein ambaye alijifunga.

Banka ameitwa kuongeza nguvu kufuatia baadhi ya viungo wa klabu hiyo kuwa majeruhi kama vile Balama Mapinduzi,Haruna Niyonzima na Papy Tshitshimbi hivyo kuilazimu klabu hiyo kumalizana na kiungo huyo haraka na tayari ameshajiunga na timu hiyo kambini mkoani Kagera kujiandaa na mechi dhidi ya Kagera Sugar.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka