Connect with us

Soka

Azam Moto,Chirwa Fire

Klabu ya soka ya Azam fc imeiwashia moto klabu ya Allince baada ya kuifunga mabao 5-0 katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliofanyika katika uwanja wa Nyamagana jioni ya leo.

Obrey Chirwa ndio alikua shujaa baada ya kufunga mabao matatu huku akifunga bao la kwanza dakika ya nne ya mchezo  huku lile la pili akapachika dakika ya 25 kabla ya Idd Chilunda kupachika bao la tatu dakika ya 33 na kuifanya Azam FC kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 3-0.

Kipindi cha pili licha ya utulivu wa Alliance,Shaban Idd Chilunda alipachika bao la tatu dakika ya 53 na baadae Chirwa alihitimisha kalamu ya mabao baada ya kufunga goli la tano dakika ya 68 na kuifanya Azam kufikisha pointi 16 za ligi kuu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka